Baadhi
ya wafanyakazi wakiwa kwenye picha ya pamoja katika sherehe ya
wafanyakazi kusherekea tuzo kubwa ya Mackay waliyoipata kutokana na
kiwanda kufanya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga
Meneja wa Kiwanda cha Bia(TBL) mkoani Mwanza, Gabriel Pitso akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati waherehe hiyo
Aliyekuwa
Meneja wa kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza, Richmond Raymond
akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa sherehe
Aliyekuwa
Meneja wa kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza, Richmond Raymond
akimkabidhi tuzo Meneja wa Kiwanda hicho, Gabriel Pitso katika sherehe
ya wafanyakazi kusherekea tuzo kubwa ya Mackay waliyoipata kutokana na
kufanya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga
Mwakilishi wa Wafanyakazi Tuico katika Kiwanda cha Bia TBL mkoani Mwanza, Vedasia Mafuru akizungumza wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia matukio wakati huo wakiburudika
……………………………………………………………………………………………………..
Wafanyakazi wa kiwanda cha TBL
Mwanza kilichopo chini ya TBL Group jana walisheherekea mafanikio
waliyoyapata mwaka huu ikiwemo kushinda tuzo kubwa ya Mackay kutokana
na kufanya uzalishaji wa kutumia teknolojia ya pumba za mpunga .
Mackay ni tuzo kubwa ya SABMiller
ya kumuenzi mmoja wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Graham Mackay
ambaye katika kipindi chake cha kuitumikia kampuni hiyo aliendeleza kwa
kiasi kikubwa na alifariki miaka mitatu iliyopita ambapo kampuni
imeanzisha tuzo yake kwa viwanda vyake ambavyo vinafanya uzalishaji
unaoendana sambamba na malengo ya kampuni .
Moja ya malengo ya SABMiller
ambayo baadhi yake yanashahabiana na malengo ya Umoja wa Mataifa
yamelenga katika kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira na
unaoleta mabadiliko kwa jamii kwa kuziwezesha kujikwamua kiuchumi.
Akiongea katika hafla
hiyo,aliyekuwa Meneja wa kiwanda hicho ambaye amehamishiwa kikazi nchini
Afrika ya Kusini,Richmond Raymond amewapongeza wafanyakazi wote kwa
mafanikio haya kwa kukiwezesha kiwanda kuendelea kungaa na kujinyakulia
tuzo mbalimbali kama hii ya Mackay.“Ushindani ulikuwa mkubwa na
ulihusisha viwanda mbalimbali lakini hatimaye tumefanikiwa kunyakua
tuzo hii na kuweka rekodi ya kuwa kiwanda cha kwanza kuipata barani
Afrika”.Alisema
Pia alitoa shukrani kwa wateja
wote wanaoendelea kuiunga mkono kampuni kwa kununua bidhaa zake na
kuongeza kuwa siku zote kampuni itahakikisha inaongeza uzalishaji na
kuendelea kuingiza bidhaa bora sokoni ikiwemo kusaidia huduma mbalimbali
zinazoleta mabadiliko kwenye jamii.
Kwa upande wake Meneja wa TBL
Mwanza Gabriel Pitso, alisema kuwa kiwanda hicho ndicho cha kwanza
kupata tuzo hii nchini na ushindi huu umetokana na kufanya uzalishaji
unaozingatia utunzaji wa mazingira kwa kutumia mashine zinazotumia pumba
za mpunga na mashudu ambao kitaalamu hujulikana kama Dry –De- Husking
(DDH) .
Alisema kampuni mama ya SABMiller
ilifanya utafiti na baada ya utafiti huo iliamua kabla ya kuanzisha
teknolojia ya uzalishaji usiotumia mafuta ya dizeli kwenye viwanda
vyake vyote ianzie katika kiwanda cha Mwanza ambapo katika miaka ya
kwanza ya majaribio mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na kutumia
teknolojia hii ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji na kupunguza
uharibifu wa mazingira.
Mbali na kupunguza athari za
uharibifu wa mazingira na gharama za uendeshaji teknolojia hii kwa kiasi
kikubwa inasaidia kuongeza vipato kwa wakulima wa pamba na mchele na
wafanyabiashara wanaokusanya pumba kwa ajili ya kukiuzia kiwanda “Zamani
pumba za mchele zilikuwa takataka lakini hivi sasa zimegeuka lulu kwa
kuwa zina soko tunazitumia katika uzalishaji hivyo kuna wafanyabiashara
wanapita maeneo mbalimbali wakizikusanya kwa ajili ya kutuuzia na huu
ndio uwekezaji mzuri unaonufaisha jamii inayoishi jirani na maeneo ya
kiwanda na ni moja ya malengo yetu”.Alisema.
EmoticonEmoticon