EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
17/7/2016
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira NEMC imekitoza faini ya shilingi milioni kumi, kiwanda
cha kutengeneza sabuni cha Royal Soap industry cha Mabibo
jijini Dar es Saal kwa kosa la kutiririsha maji machafu na yenye sumu sambamba
na vumbi la sabuni lenye kusambaa katika makazi wa watu na mazingira ya mto
kibangu.
Uchafuzi huo wa mazingira umekuwa ni wa muda
mrefu katika makazi ya mtaa wa mabibo kisimani na kupelekea afya za wakazi wa
eneo hilo kuwa hatarini, kutokana na maji machafu yenye kemikali na vumbi la
sabuni, na kupelekea wananchi wa mtaa huo wa kibangu kupeleka malalamiko yao
katika Ofisi ya Makamu wa Rais, na ndipo
Naibu Waziri wa Ofisi Hiyo anaeshunghuliakia masuala ya Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Joelson Mpina, kuinuka ofisini
na kwenda kujionea adha wanayoipata wakazi hao.
Naibu Waziri Mpina alilielekeza Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuatilia vipimo vya vumbi na maji
ya sabuni yanayotiririka katika mazingira na mto kibangu, kama ni rafiki kwa
mazingira na viumbe hai na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne sanjari na kukitoza faini ya shilingi milioni
kumi kiwanda hicho na kukitaka kilipe kwa muda huo wa wiki mbili, kwa kosa la
kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zaake ya mwaka 2004.
Naibu Waziri Mpina, yupo kwenye ziara ya ukaguzi
wa mazingira na kufuatiliaji na uzingatiaji wa sheria ya mazingira na kanuni
zake kwa wawekezaji wenye viwanda nchini. Amewashukuru wananchi kwa kuripoti
moja kwa moja kwa serikali juu ya waharibifu wa mazingira, na kuonyesha kuwa
malalamiko ya wananchi yanafanyiwa kazi, Naibu Waziri Mpina anafanya Ziara
nyingi za kushtukiza katika viwanda.
EmoticonEmoticon