Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF
Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
Idara ya Habari maelezo leo kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na
mfuko huo katika huduma zake mbalimbali nchini kwa jamii Kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF
Bw. James Mlowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano
huo.
……………………………………………………………………………………………………………….
HASSAN SILAYO
Mfuko wa Pensheni wa LAPF
umefanikiwa kusajili wanachama wapya 27, 362 katika mwaka wa fedha wa
2014/2015 tofauti na mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo walisajili
wanachama 23,228.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Elimu
na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe wakati na
mkutano wa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Mlowe alisema kuwa mafanikio
hayo yanatokana na huduma na mafao bora yenye wigo mpana na kugusa moja
kwa moja maisha ya mtanzania ambapo wamepanga kufikia wanachama 180,000
kufikia mwezi June 2016.
Mlowe aliongeza kuwa miongoni mwa
sekta zilizoingiza wanachama wapya kwa mwaka 2014/2015 ni Walimu
ambapo imetoa wanachama 39,537, Zimamoto na uokoaji wanachama 851,
Polisi na Uhamiaji wanachama 415 na Magereza wanachama 205.
Aidha Bw. Mlowe aliongeza kuwa
katika kipindi cha mwaka 2014/2015 mfuko huo ulikusanya kiasi cha
shilingi bilioni 210.069 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.9, ambapo
wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 286 billioni kufikia
mwezi Juni 2016.
Pia Mfuko huo umesajili waajiri
wapya 88 katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na unategemea kuendelea
kuongezeka siku hadi siku kutokana na mfuko huo kuendelea kuboresha
huduma zake.
EmoticonEmoticon