Mtaalam
Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero
akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni
Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez
akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto
ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa
Ero.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame
Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa
Ngozi, Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
……………………………………………………………………………………………………………
Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Pamoja na juhudi ambazo
serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino
wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya
hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango
kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu
ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa
Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa
ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi
ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
“Tangu nimeingia sijawahi
kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua
sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi
mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu
walio na uablino,” alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano
hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili
kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
“Tumejadili mambo mengi lakini
tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na
ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia
waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino,”
alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja
wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez
alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha
kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
EmoticonEmoticon