Akitaja
vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na
waanzilishi wa Maisha Plus alisema, “Tunachukua washiriki wenye umri wa
miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia
kutoka nchi za Afrika Mashariki”
Maisha
Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi
tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo
mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya
kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni
‘Vijana Ndio Ngazi’.
Usaili
unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania.
Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio
mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali
ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv
EmoticonEmoticon