Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni mfanyabiashara
aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika
kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani
Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na
kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mfanyabiashara
John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo
katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali
aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa
kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara
ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na
wahamiaji haramu kuingia nchini. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu
wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono),
akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya
Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia
zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kulia), akipanda Mlima kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya
Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani
Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi
ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji
haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Ujumbe
ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka mlimani baada ya ukaguzi
wa mpaka uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo
mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na
kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
EmoticonEmoticon