Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo akionyesha jinsi watumiaji wa mtandao wa Cheki.co.tz jinsi wanavyoweza kutumia huduma ya clearing and forwarding.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria
mkutano huo wakiendelea na kazi yao ya kuchukua taarifa kwa ajili ya kuupasha
umma kuhusu huduma ya clearing and forwading ambayo inatolewa na cheki.co.tz
Mtandao
wa kuuza magari mtandaoni wa Cheki.co.tz umezindua huduma mpya ya uunganishwaji
wa uigizaji magari kutoka nje ya nchi na huduma ya utoaji magari bandarini
(clearing and forwarding), huduma ambayo itawarahisishia wananchi ambao
wanaagiza magari nje ya nchi kuwa na uhakika wa usalama wa magari wanayoagiza
mpaka yanakapowafikia.
Akielezea
huduma hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Cheki Tanzania, Mori Bencus, alisema
kampuni yake imeanzisha huduma hiyo ili kuwarahisishia Watanzania wanaoanzisha
magari nje ya nchi kutokana na kubaini kuwa wamekuwa wakisumbuka kukamilisha
uagizwaji wa magari na kuyatoa bandarini.
“Tayari
tumewapa wateja wetu chaguo kubwa la magari kutoka kwa wauzaji wa kuaminika
kutoka nje ya huduma hii ya utoaji wa mizigo itarahisisha utoaji wa magari
kutoka bandarini na hivyo wateja kupunguza gharama na muda wa kusubiri,” alisema
Bencus.
Nae
Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo, alisema kuwa kampuni hiyo
haihusiki na uuzaji wa magari ila inachofanya ni kumuunganisha mnunuzi wa gari
na muuzaji ili waweze kufanya biashara kwa haraka na urahisi zaidi.
Ujio
wa huduma hiyo imekuwa mwendelezo wa uboreshwaji wa huduma za ununuzi wa magari
kwa kupitia mtandaoni ambazo zinafanywa na mtandao wa Cheki.co.tz ambao
unafanya kazi na wauzaji wa magari wa kimataifa wa nje ya nchi na wauzaji
wa magari wa hapa nchini.