Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey
Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo
kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es
salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa
kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza
msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka
Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto
wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo
jijini Dar es salaamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Fundi mitambo Bw.
Simon Dotto kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta
kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika
hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa
kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika
kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka
kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Beatrice Lyimo)
EmoticonEmoticon