Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Elius Mwakalinga akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu kutekelezwa kwa mpango wa
Serikali wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora
ambapo wakala huo unajenga nyumba 10,000 ili kutimiza azma hiyo. Kulia
ni Mkurugenzi wa Milki Bw. Baltazar Kimangano na kushoto ni Mkurugenzi
wa Ushauri Bw. Edwin Nnunduma.
Mhandisi
Ujenzi kitengo cha Upimaji na Ukaguzi Majengo toka Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) wakwanza kulia Bi Khadija Salum akionesha kwa waandishi
wa Habari sehemu ya vifaa vilivyonunuliwa na wakala huo kwa ajili ya
kupima ubora wa majengo yaliyokwisha jengwa na yale yanayoendelea
kujengwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na majengo yenye ubora
kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
( Picha na Habari na Frank Mvungi ).
………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kupitia wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) imenunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila
kuyaharibu (Non destructive Testing equipments) .
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es
salaam na Mtendaji Mkuu waTBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano na
vyombo vya Habari uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo.
Akifafanua Mwakalinga amesema kuwa
wakala huo umenunua vifaa vya kisasa ili kuwezesha ukaguzi wa ubora wa
Majengo ya Serikali ili kuwa na majengo yenye Ubora unaotakiwa.
“Lengo la kununua vifaa hivi ni
kuhakikisha kuwa majengo yote ya Serikali yanakuwa na ubora kwa kuwa
tutayapima yaliyopo na yale yanayojengwa ili tuweze kuchukua hatua pale
inapodi” alisisitiza Mwakalinga.
Akieleza umuhimu wa vifaa hivyo
Mwakalinga amesema kuwa hakutakuwa na wasiwasi tena kuhusu uwezekano wa
wakandarasi kudanganya wakati wa ujenzi.
Aidha vifaa hivyo vitawezesha
Wakala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya Serikali ili
kubaini hali ya ubora wa majengo hayo ambapo gharama ndogo za ada ya
ushauri zitatozwa kwa Taasisi husika.
Vifaa hivi ni kama Rebund hammer
inayotumika kupima uimara wa zege iliyokauka, cover meter kwa ajili ya
kupima ukubwa wa nondo na umbali uliowekwa.
Akitaja vifaa vingine Mwakalinga
amesema kuwa ni “Utrasonic system/testing device” kwa ajili ya kupima
muonekano wa ndani ya zege iliyokauka.
Mbali ya jukumu la kuhakiki ubora
wa majengo ya Serikali, Wakala umeendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba
zinazouzwa kwa gharama nafuu kwa watumishi wa umma ambapo mpango wa
wakala huo ni kujenga nyumba elfu kumi katika maeneo mbalimbali hapa
nchini.
EmoticonEmoticon