Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi
ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi
Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa
DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu
ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali
zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili
ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.
Usafiri DART umekuwa mkombozi
kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani
mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia
jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua
kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika
kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza
swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo
wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia
utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto
zinazojitokeza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikaua kituo cha Kimara Mwisho.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia
jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David
Mwaibula.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu hiyo leo kulia
ni Mzee David Mwaibula na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
EmoticonEmoticon