Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati), Naibu Katibu Mkuu Angelina Madete (kulia) na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii
Wilfred Msemo (kushoto) wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa “Solidarity
Forever” wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi la
Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana tarehe 17 Mei, 2016
katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, tawi la Bustani, Jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi
akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi
Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha
Taifa cha Utalii, Jijini Dar es Salaam.
Katika
salamu zake amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa
wanatimiza wajibu wao katika kutekeleza lengo kuu la Wizara ambalo ni
kuendeleza uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kukuza Utalii nchini.
Amewataka
watumishi wote wa Wizara kuwa waadilifu, wabunifu, kufanya kazi kwa
ushirikiano, kuepuka vitendo vya rushwa na makundi yasiyokuwa na tija
kwa Wizara na Serikali kwa ujumla.
Alionya
kuwa, Mtumishi yeyote atakeenda kinyume cha sheria na taratibu hatosita
kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi ili kwenda
sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya “HAPA KAZI TU”
Maj.
Gen. Milanzi alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe ambaye yupo Mkoani Dodoma kwa ajili ya majukumu
mengine ya Kiserikali (Bunge la bajeti).
Sehemu
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii
wakiimba wimbo wa kuashiria umoja wa wafanyakazi (Solidarity Forever).
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakiimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi “Solidarity Forever”
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)
EmoticonEmoticon