MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba
Omar Khamis Othman amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya pamoja
na Baraza la Mji Wete , ambaye atashindwa kutekeleza wajibu wake ,
atatumia nguvu alizonazo kisheria kumuweka rumande masaa 24 , kwani
atakuwa ni chanzo cha kukosekana mapato ya Serikali .
Aliesema kuwa ni wajibu wa kila
mfanyabiashara kukata leseni za biashara yake ili aweze kuchangia
mapato ya Serikali Kuu ambayo baadaye hurejea kusaidia miradi ya
maendeleo ya wananchi .
Alisema kuwa mapato ya Serikali
hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na ukusanyaji wa mapato
kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa muhali , jambo ambalo
alisema serikali ya Mkoahaitalivumilia.
Kauli hiyo ameitoa wakati
akizungumza na watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Wete na Micheweni ,
watendaji wa Baraza ka Mji wete pamoja na watendaji kutoka Serikali za
Wilaya juu ya kuimarisha suala la ukusanyaji wa mapato
Aidha aliwataka wakurugenzi wa
Halmashauri za Wilaya na Baraza la Mji Wete kuondoa muhali katika suala
la ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha wafanya biashara wanakata
leseni za biashara zao.
“Ninao uwezo na nguvu kisheria
wa kumweka rumande mtumishi wa Serikali masaa 24 , ambaye atashindwa
kutekeleza wajibu wake , mimi sitangoja kutumbuliwa jipu nitaanza na
atakaye onyesha uezembe katika agizo hili ”alieleza.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa
mapato ya Serikali hupotea kutokana na watendaji wanaohusika na
ukusanyaji wa mapato kushindwa kuwajibika kutokana na suala la rushwa
muhali , jambo ambalo amesema haitalivumilia .
Pia aliwataka kutumia lugha
nzuri kwa wateja wao kwa kuwaelimisha , na wakiendelea kukaidi
wawafiishe ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa hatua zaidi .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Micheweni Abeid Juma Ali amewasisitiza watendaji wa Halmashauri na
baraza la Mji kufuata sheria na miongozo wakati wanapotekeleza majukumu
ya kazi zao
Alisema kwamba iwapo sheria
zitatumika ipasavyo kila mfanyabiashara atakata leseni yake bila ya
usumbufu na kuwasisitiza kuwachukulia hatua wanaoendesha biashara bila
ya kuwa na leseni .
“Sheria zipo lakini hazitumiki ,
zitumieni kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara abakuwa na leseni na
ambaye anakiuka mchukulieni hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kumfikisha mahakamani ”alifahamisha .
Akichangia katika Mkutano huo ,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Wete Mmanga Juma Ali alisema ili
kuzipatiwa ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanahitaji kupatiwa askari
watakaoongozana nao kupita madukani na kudai leseni .
Alisema kuwa kipindi cha
vuguvugu la kisiasa , mapato ya Halmashauri yamepungua kutokana na
wafanyabiashara wengi kuendesha biashara bila ya kukata leseni .
EmoticonEmoticon