Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati),
akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Aggrey Mwanri
(kushoto), wakati alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Tabora Mjini, Bw. Suleiman Kumchaya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifafanua
jambo wakati akiongea na Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara
yake Mkoani Tabora.
Mkuu
wa Wilaya ya Nzega, Bi. Jacqueline Liana (kulia), akimsikiliza kwa
makini Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (katikati), Profesa
Makame Mbarawa wakati alipomtembelea ofisini kwake kuhimiza matumizi ya
mifumo ya kielektroniki, mawasiliano ya simu na Internet katika Ofisi za Serikali, Wilayani hapo.
Muonekano
wa kichwa kipya cha Treni kabla ya kuanza safari katika stesheni ya
Tabora. Uwepo wa hivyo vipya unatarajiwa kuongeza kasi ya usafirishaji
wa abiria na mizigo katika reli ya kati.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikagua
kifaa maalum cha kupimia mafuta kilichofungwa kwenye kichwa kipya cha ya
Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mkoani Tabora.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wa Tabora, Eng.
Damiani Dabalinze, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokagua ujenzi wa
barabara ya Itigi-Tabora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa , akielekea
kukagua nyumba za zitakazovunjwa kupisha upanuzi wa barabara
Tabora-Itigi, Mkoani Tabora.
…………………………………………………………………..
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa siku
nne kwa Kampuni ya Reli Nchini (TRL) kuondoa uzio wake katika eneo la
hifadhi ya Barabara ya Itigi-Tabora ili kupisha ujenzi wa Barabara hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kukagua barabara hiyo, Prof. Mbarawa amemtaka Meneja wa
TRL kanda ya Tabora, Bw Gukwi Marko kuhakikisha uzio huo unaondolewa
mara moja ili barabara hiyo ijengwe na hivyo kurahisisha usafiri
katikati ya mji wa Tabora.
“Meneja
hakikisha uzio huu unasogezwa na TANROADS wanaanza ujenzi wa barabara
mara moja, Hatuwezi kuchelewesha maendeleo ya wanannchi kwa sababu ya
mivutano isiyo na tija”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa ameagiza nyumba tatu zinazomilikwa na Kampuni Miliki ya
Rasilimali ya Reli (RAHCO) kubomolewa mara moja ili kupisha ujenzi huo
na kuwaagiza RAHCO kufatilia malipo yaliyolipwa na TANROADS.
Katika
Hatua nyingine amezitaka taasisi 29 zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya
kazi kwa pamoja na kuhakikisha zinatumia huduma zinazotolewa na taasisi
hizo ili kukuza uchumi ndani ya taasisi hizo.
“Naagiza
taasisi zote 29 zilizo chini ya Wizara ziunganishiwe huduma ya simu ya
TTCL, na zote zipeleke magari TEMESA ili kuinua uchumi ndani ya Wizarara
na hivyo kunufaika na fursa ya kuwa ndani ya wizara moja”,amesisitiza
Waziri Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amezitaka taasisi zilizo chini ya wizara yake kutambua fursa ya
kuwa ndani ya wizara moja na hivyo kuitumia ili kunufaika kibiashara na
kiutaalamu.
Aidha
ametoa onyo kwa wananchi kuepuka vitendo vya hujuma dhidi ya
miundombinu ya mawasiliano hususani nyaya za mkongo wa taifa ambazo
licha ya nyaya hizo kutokuwa na thamani ya shaba wala dhahabu pia ni
hatari kwa usalama kwani zinaweza kuhatarisha maisha.
Waziri
Prof. Mbarawa amehitimisha ziara yake ya siku saba katika mikoa ya
kanda ya Magharibi na kuwataka viongozi wa Serikali na taasisi zilizo
chini ya wizara yake kufanya kazi kwa pamoja ili kufungua mikoa ya
Kigoma, Katavi, Rukwa na Tabora.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
EmoticonEmoticon