Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Mbeya wakichukua kumbukumbu za Mkutano huo.
SERIKALI Mkoni Mbeya, imezirejesha
hekta 5000 za ardhi ya kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali, zilizokuwa
zimetolewa kwa wakulima zaidi ya 200 wa chama cha Luhanga (Luhanga AMCOS), huku
ikiuagiza uongozi wa halmashauri kuwachukulia hatua watendaji wote walihusika
na mchakato wa ugawaji wa ardhi hiyo.
Akikabidhi ardhi hiyo leo, kwa
wananchi wa Kata ya Luhanga, Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi
Makala, alisema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kwamba zoezi hilo
lilifanyika kinyume na sheria na kanuni za ardhi za vijiji
zinavyoelekeza.
Amesema, sheria mama namba 5
ya ardhi ya mwaka 1999, imebainisha kwamba halmashauri ya kijiji haina mamlaka
ya kugawa ardhi zaidi ya ekali 20 au 50 lakini wao wamegawa ardhi zaidi ya
hekta 5000.
Mkuu huyo ameongeza kuwa mbali na
zoezi hilo kughubikwa na ukiukwaji wa sheria lakini pia, wawekezaji hao
wameonekana ni wababaishaji kutokana na kushindwa kutimiza ahadi za
maendeleo walizokuwa wamezitoa kwa wananchi wa eneo hilo.
Aidha, Makala, aliwatahadharisha
wananchi hao, kujiepusha na walaghai wa ardhi na kuacha kugawa ardhi ovyo kwani
rasilimali hiyo haiongezeki ukilinganisha na mahitaji ya watu, ambao kila siku
wanaongezeka idadi.
Amesema serikali inaweza kufanya uparesheni ya kuwataka vijana wafanye kazi lakini kama wananchi au viongozi wanauza ardhi zoezi hilo haliwezi kufanikiwa .
Amesema mkoa wa mbeya unajulikana kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi hususani wilaya ya mbarali hivyo yeye kama mkuu wa mkoa atahakikisha anashughulika vyema na suala hilo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka jamii za wafugaji wa kimasai kuhakikisha wanaachana na tabia ya kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo badala yake wawalitihishe katika elimu ambayo ndio mkombozi kwao.
Mwisho.
Habari hii imeandaliwa na mtandao wa kijamii wa www.jamiimoja.blogspot.com-0759406070 Mbeya.
|
EmoticonEmoticon