TANGAZO KWA UMMA.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Jafary Michael (Chadema)
anatoa tahadhari kwa umma ya kuwa kuna baadhi ya watu wenye nia mbaya wanatumia
namba yake ya simu ya mkononi ya mtandao
wa Vodacom kufanya utapeli .
Watu hao wamekuwa wakituma
ujumbe mfupi (SMS) kwa watu mbalimbali kwa lengo la kutapeli wakiomba kutumiwa
fedha .
Wakati akishughulikia suala hilo
katika vyombo vya dola ametoa ombi kwa yeyote atakayepata ujumbe huo kuupuza na
kutoa taarifa kwa yeyote atakaye fikwa na kadhia hiyo.
Ukipata ujumbe huu mfahamishe na
mwenzako.
Imetolewa na :
Japhary Michael
Mbunge wa Moshi mjini
EmoticonEmoticon