mbunge wa Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto akisalimiana na wananchi wa Ilula waliokuwa wakisubiri maji
Mwamoto akizungumza na meneja wa maji mji mdogo wa Ilula Bi Mvungi |
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto (kushoto) akisalimiana na mmoja kati ya wazee wa mji wa Ilula aliyetoka kuchota maji
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akisaidia kufungulia maji |
……………………………………………………………………………………………………………………..
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ameahidi kuongozana na wazee
wa mji wa Ilula kwenda Dodoma kuonana na waziri mkuu
Kassim Majaliwa ili kumfikishia ahadi ya maji ya Rais Dr John
Magufuli kwa
wananchi wa mji mdogo wa Ilula .
wananchi wa mji mdogo wa Ilula .
Huku
akiwataka wananchi wa Ilula na Nyalumbu kutomchagua mwaka 2020
iwapo atashindwa kutekeleza ahadi ya maji katika mji huo wa Ilula
ndani ya miaka yake mitano ya ubunge.
Akizungumza
na wananchi wa kata ya Nyalumbu na Ilula wakati wa mikutano
yake ya hadhara ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kuwa
mbunge wa jimbo hilo la Kilolo jana ,Mwamoto alisema kuwa kero ya
maji
katika mji wa Ilula imekuwa ya muda murefu jambo ambalo hatataka kuona wananchi hao wakiendelea kutabika.
katika mji wa Ilula imekuwa ya muda murefu jambo ambalo hatataka kuona wananchi hao wakiendelea kutabika.
Alisema
kuwa kero hiyo ya maji imeanza kuwasumbua wananchi hao toka
nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 hadi leo wapo katika mahangaiko ya
maji na baadhi ya viongozi wameendelea kufanya udanganyifu wa mradi
huo
kama ambavyo mwaka 2010 viongozi walivyomdanganya aliyekuwa makamu wa Rais Dr Alli Mohamed Shein kwa kupelekwa kufungua mradi wa maji ambao viongozi walimdanganya kwa kujaza maji katika tanki
hilo ili azindue mradi huo.

Hivyo
alisema udanganyifu huo hautapewa nafasi katika uongozi wake
wa miaka mitano lazima kero hiyo imalizike na wananchi hao
waweze kupata maji vinginevyo yupo tayari kuongoza wananchi wake
kumzuia waziri wa maji kupita Ilula kwenda jimboni kwake Njombe iwapo
wananchi hao hawatatimiziwa ahadi yao ya maji safi na salama .
Mbunge
huyo alisema katika kikao kijacho cha bunge kinachoanza mwezi
ujao ataomba wananchi wa Ilula na Nyalumbu kumteulia wazee watatu ama
wanne ili kwenda nao bungeni Dodoma kukutana na waziri mkuu ili
kwa ajili ya kumkumbusha ahadi ya Rais ya maji katika mji huo wa Ilula
kwa ajili ya kumkumbusha ahadi ya Rais ya maji katika mji huo wa Ilula
Pia
aliagiza mamlaka ya maji ya mji mdogo wa Ilula kuchunguza vema
mradi wa maji uliopo kama umejengwa kwa kiwango ama chini ya kiwango
maana amesema mradi mdogo uliopo kwa sasa bado umekuwa na kero kubwa
ikiwa
ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji huku akiwataka wananchi kwa upande wao kutunza miundombinu ya maji.
ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji huku akiwataka wananchi kwa upande wao kutunza miundombinu ya maji.
Katika
hatua nyingine mbunge Mwamoto alimshauri meneja wa maji wa
IRUWASA katika mji wa Ilula Teodolah Mvungi kuangalia uwezekano wa
kuboresha kituo cha maji eneo la Ilula ili kiweze kunufaisha
wananchi wengi
na kuwa iwapo wataanza uboreshaji kwa upande wake ataunga mkono .
na kuwa iwapo wataanza uboreshaji kwa upande wake ataunga mkono .
EmoticonEmoticon