Kamishna Jenerali wa Magereza –
CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili Mwamugunda alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani
Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea eneo kunakojengwa Gereza la
Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita pamoja na Gereza la Wilaya ya
Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya
Magereza Mkoani Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja na Luteni Jenerali Mstaafu
Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha Busisi kabla ya kuendelea
na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani
Mwanza, Goleha Masunzu.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe.
Shaban Ntarambe(kushoto) akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya wakielekea eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato mara baada
ya Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasili Wilayani Chato kabla ya
kuelekea Mkoani Kagera
Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Omar Mtiga(wa pili kushoto)
akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu
kulia) nyumba mbili za Askari wa Jeshi la Magereza ambazo tayari
zimekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wa
pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe.
Kamishna Jenerali wa Magereza,
John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia moja ya Bweni la kulala
Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika katika eneo linakojengwa
Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Kukamilika kwa Gereza hilo
kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu katika
Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
Kamishna Jenerali wa Magereza
John Casmir Minja akisaini katika kitabu cha Wageni alipotembelea Gereza
la Wilaya ya Biharamulo katika ziara yake ya kikazi leo Machi 10, 2016.
Mkuu wa Gereza la Biharamulo,
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion Kakulu akimuonesha Kamishna
Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya Gereza hilo katika ziara yake
ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi
hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara
yake ya kikazi.
EmoticonEmoticon