Watanzania watakiwa kutumia mobile banking kukuza uchumi wao

April 13, 2016

DSC_0093
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kutokana na kukua kwa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi (mobile banking), Watanzania wametakiwa kutumia nafasi hiyo vizuri ili iweze kuwasaidia kukuza uchumi wao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku mbili unaozungumzia maendeleo ya sekta za fedha kwa kutumia mifumo ya huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu (Africa Digital Banking Summit), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema ni muda muafaka kwa Watanzania kutumia huduma hizo kwa ajili ya kujiongezea kipato.
Alisema kupitia huduma hizo, Watanzania wanaweza kutuma nakupokea pesa kutoka maeneo mbalimbali hata ambayo yapo mbali na matawi ya benki hivyo wanaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwepo kufanya biashara kwa kutumia huduma hizo.
“Serikali imeunganisha nchi nzima na mkongo wa taifa na hii inawapa fursa watanzania kutuma pesa sehemu yoyote hivyo niwasihi watanzania kutumia kikamilifu nafasi hiyo ili kuboresha uchumi wao,” amesema Dkt. Kijaji.
DSC_0032
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba katika mkutano huo. (Picha zote na Rabi Hume, Modewjiblog)
Nae Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema kuwepo kwa huduma za kibenki kupitia mitandao ya simu kumewezesha wateja wao kupata huduma kirahisi tofauti na miaka ya nyuma kabla ya kuanza kwa huduma ya mobile banking.
Alisema kupitia huduma hiyo kwa sasa wateja wao wanauwezo wa kutoa fedha, kulipia huduma mbalimbali kama kodi, kununua umeme, tiketi za ndege na hata kuangalia salio lililo katika akaunti zao za benki na wanachokifanya kwa sasa ni kuangalia jinsi gani wanaboresha zaidi huduma hizo kwa wateja hasa walio maeneo ya vijijini.
“Miaka ya nyuma kama mteja yupo kijijini anatumia muda mwingi kwenda sehemu iliyo na huduma ya benki lakini kwa sasa huduma za kibenki katika mitandao ya simu imerahisisha hata wateja wetu walio vijijini kupata huduma zetu kiurahisi,” amesema Bi. Bussemaker.
DSC_0061
Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumza katika mkutano huo.
Nae Meneja wa Mifumo wa Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi amesema huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu imekuwa ikizidi kukua siku baada ya siku tangu ilipoanza nchini mwaka 2008 na mpaka sasa kuna benki 30 ambazo zimejiunga katika mfumo huo ili kuwasogezea huduma wateja wake.
DSC_0043
Meneja Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi akitoa taarifa kuhusu matumizi ya mobile banking nchini.
DSC_0015
Mwongozaji wa mkutano huo, Chris Mauki.
DSC_0026
Mwenyekiti wa mkutano wa Africa Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu akizungumza kuhusu mkutano huo.
DSC_0029
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili.
DSC_0051
Pia Mkurugenzi Mkakati wa Jackson Group Ltd, Kelvin Twissa ni mmoja wa washirikia waliohudhuria mkutano huo (wa kwanza kulia).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »