Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la
kheri timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao ya kimataifa
inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
TFF imezitaka Azam FC na Yanga kupambana katika michezo yao ugenini
ili kupata matokeo mazuri yatakayozifanya ziweze kusonga mbele katika
hatua inayofuata, ikiwa kwa sasa ndio wawakilishi pekee wa Tanzania
katika michuano ya kimataifa.
Azam FC inayoshirki michuano ya Kombe la Shirkisho barani Afrika (CAF
CC), leo saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki inashuka dimba la
Olymique 07 November, Rades jijini Tunis kuwakabili wenyeji Esperance ST
katika mchezo wa marudiano.
Kesho Jumatano, Yanga SC watakuwa ugenini kuwakabili wenyeji Al Ahly
SC katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF
CL), mchezo utakaochezwa saa 2:30 usiku katika uwanja wa Borg El Arab
kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.