Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama, Nyamisati -Rufiji
Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf, Mitwero Lindi
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatangaza nafasi za
kidato cha kwanza kwa wasichana katika Shule zake mbili za Sekondari:
(1) Shule ya Sekondari WAMA – Nakayama iliyopo Kijiji cha Nyamisati Wilaya ya Rufiji , Mkoa wa Pwani:
(2) Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf iliyopo Mitwero katika Manispaa ya Lindi
(2) Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf iliyopo Mitwero katika Manispaa ya Lindi
WAMA ni Taasisi isiyo ya
kiserikali iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia
maendeleo ya wanawake na watoto. WAMA inaendesha shule hizi maalum kwa
ajili ya watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu. Hata hivyo,
WAMA inatoa fursa chache kwa wanafunzi wengine ambao wazazi wao wana
uwezo wa kulipia ili kuongeza uwezo wa kusaidia watoto wengi zaidi.
Tunafurahi kutoa fursa hii kwa
wasichana ambao wataweza kulipia ada kwa kidato cha kwanza katika shule
zote mbili kwa mwaka 2016.
Fomu za kujiunga zinapatikana
katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam
zilizopo Kawe karibu na Hoteli ya Picolo Beach au katika Tovuti ya
Taasisi: www.wamafoundation.or.tz
Kwa wakazi wa Lindi fomu zinapatikana katika Ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) tawi la Lindi zilizopo katika makutano ya Barabara ya Karume na Amani , Kiwanja no.11 kitalu B karibu na Ofisi za Magereza za Mkoa wa Lindi
Kwa wakazi wa Lindi fomu zinapatikana katika Ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) tawi la Lindi zilizopo katika makutano ya Barabara ya Karume na Amani , Kiwanja no.11 kitalu B karibu na Ofisi za Magereza za Mkoa wa Lindi
Kwa Dar es Salaam mtihani wa
kujiunga na shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika
Alhamisi Novemba 12, 2015 katika Shule ya Sekondari Jangwani.
Kwa Lindi mtihani wa kujiunga na
shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika Alhamisi Novemba
19 , 2015 katika Chuo cha VETA Lindi.
Mwanafunzi anatakiwa arudishe fomu
pamoja na risiti ya malipo katika ofisi za Taasisi ya WAMA au kwa
kutumia barua pepe: info@wamafoundation.or.tz, mbugunimwajuma@gmail.com
na alimindria66@yahoo.com. Mwisho wa kurudisha fomu ni Jumatano tarehe
11 Novemba, 2015.
Shule zetu zina mazingira na
huduma zote muhimu zinazowawezesha wanafunzi kufaulu vizuri yakiwemo
mabweni ya kisasa, maabara za kisasa, maabara za computer, maktaba zenye
vitabu vya kutosha na walimu wazuri na wakutosha.
Kwa Mawasiliano zaidi:
Piga Namba: 0685-651449, 0789-000341, 0754-439183,
Barua pepe: info@wamafoundation.or.tz
Tovuti: www.wamafoundation.or.tz
Piga Namba: 0685-651449, 0789-000341, 0754-439183,
Barua pepe: info@wamafoundation.or.tz
Tovuti: www.wamafoundation.or.tz
EmoticonEmoticon