STEWART HALL: MBIO ZA UBNGWA SASA ZIMESHIKA KASI AZAM FC

October 30, 2015

MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Oktoba 31, 2015
Simba SC Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs Mwadui FC
Prisons Vs Ndanda FC
Coastal Union Vs Mbeya City
Novemba 1, 2015
African Sports Vs JKT Ruvu
Azam FC Vs Toto Africans
Novemba 2, 2015
Mgambo Shooting Vs Stand United

Kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Hall amesema mbio za ubingwa sasa zimeshika kasi katika timu yake

Na Princess Asia,  DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu Azam FC, Muingereza Stewart John Hall amesema kwamba anataka kuendeleza wimbi la ushindi ili kuhakikisha anatimiza ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam FC jana imepanda kileleni kwa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, hivyo kufikisha pointi 22, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC, baada ya timu zote hizo kucheza mechi nane.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jana, kocha huyo aliyeipa Azam FC ubingwa wa Afrika Mashariki, Kombe la Kagame Agosti mwaka huu, amesema kwamba lengo si kuwa kileleni mwa Ligi Kuu kwa muda, bali kutwaa ubingwa.
“Si suala la kuwa juu tu, nataka kufikia malengo tuliyojiwekea, hivyo kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha tunapata pointi tatu za kila mechi tutakazocheza,” alisema.
John Bocco jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-2 wa Azam FC

Stewart amefurahishwa na safu yake ya ushambuliaji kwa kucheza kwa ‘njaa ya kufunga’ na kufuata maelekezo anayowapa kabla ya mchezo.
“Nina imani na safu yangu ya ushambuliaji, kama bao la nne lililofungwa na Kipre Tchetche ni la aina yake, ile ilikuwa moja ya maagizo niliyomuagiza na kufanyia kazi,” amesema.
Azam FC inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumapili kumenyana na Toto Africans katika mfululizo wa ligi hiyo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea mwishoni mwa wiki, Jumamosi Simba SC ikimenyana na Majimaji FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga SC na Kagera Sugar Uwanja wa Mwinyi, Tabora, Mtibwa Sugar na Mwadui FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Prisons na Ndanda FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Coastal Union na Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mechi nyingine zitachezwa Jumapili, na mbali ya Azam FC na Toto, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga African Sports itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu wakati Jumatatu, Mgambo Shooting itaikaribisha Stand United Uwanja wa Mkwakwani.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »