RAILA ODINGA AMPONGEZA DKT MAGUFULI,AMSHAURI LOWASSA AENDE MAHAKAMANI KAMA HAJARIDHIKA

October 30, 2015
Waziri Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.

Akiongea katika mahojiano na BBC, Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Ameeleza pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la nchi hizo.

chanzo:Michuziblog

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »