Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waandi wa habari wapo picha juu ya ujenzi
wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na
Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.kikao hichi kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza juu ya ujenzi huo na Mjumbe
kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais
Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na Mjumbe
kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais
Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbarimbari na Mjumbe
kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais
Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
WAZIRI
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe
amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi
wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba
kwenye maeneo ya mji huo.
Akizungumza
na wandishi wa habari badaa ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya
China Merchants Group itakayosimamia ujenzi huo, Dk Hu Jianhao, Membe
alisema katika ujenzi huo utakaochukua hekta 2400, wananchi wote
watakaohuswa hawataachwa bure.
“Mradi
huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group,
wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali
ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa
na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi
zaidi na kuzalisha ajira nyingi,” alisema.
Mradi
mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa
bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.
Mazungumzo
hayo ni sehemu ya awali ya maandalizi kwa ajili ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa bandari hiyo, katika sherehe inayotarajiwa
kuongozwana Rais Jakaya Kikwete leo.
Mradi
huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika
Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 10 na
kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka jana, Rais Kikwete ataweka jiwe
hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi huo.
Eneo
hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania,
Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa
Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).
Chini
ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya
Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje
(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.
Dk
Turuka alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile
reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na mitandao ya
mawasiliano.
Mradi
huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji
kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na
viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.
Kwa
mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano wa
muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika
kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza
ajira nchini.
mwaka 2008, Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.
Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.
Wengine
wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani
wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo,
Shehe Abdullah Al Saadi.
EmoticonEmoticon