CHADEMA, NCCR-MAGEUZI WASHIKANA MASHATI VUNJO

September 20, 2015

HALI ya Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (UKAWA), si shwari ndani ya Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kutokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na NCCR-Mageuzi kushindwa kuheshimu makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja kwa kila kata.
Hali hiyo imekuja baada ya wagombea udiwani wa Chadema kukataa kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo hilo NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye amesimama chini ya mwavuli wa Ukawa kwa madai kuwa, amekiuka makubaliano ya umoja huo.
Wagombea hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, katika kipindi hiki cha kampeni, hawatamnadi mgombea ubunge wa Ukawa wakidai hata yeye mgombea ubunge amekuwa akiwapiga vita wagombea udiwani wa Chadema.
Mmoja wa madiwani hao, ambaye ni mgombea wa kata ya Mamba Kusini, Fredy Shayo, alisema hali hiyo imetokea baada ya vyama hivyo kushindwa kuelewana katika makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja, ambapo Chadema na NCCR-Mageuzi vimesimamisha wagombea wao wa udiwani kwenye kata zote 16 za jimbo la Vunjo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »