Muwakilishi wa Shirika la Afya
Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate akuitoa hotuba ya
ufungua wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na utoaji
wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali katika
ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu
unaoendelea jijini Nairobi.
Baadhi
ya washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na
utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali
katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa siku tatu
unaoendelea jijini Nairobi.
Muwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchi Kenya Dkt. Custodia Mandlhate
(aliyesimama katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
washiriki wa semina ya inayohusu namna ya kuimarisha mawasiliano na
utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya mafua makali
katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika mara baada ya
ufunguzi wa Semina hiyo.
…………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Nchi za Afrika zimeaswa
kuimarisha mawasiliano katika utoaji wa taarifa zinazohusiana na
magonjwa ya mafua makali yanayosababishwa na virusi vya influenza ili
kuokoa maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa hayo.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya Dkt. Custodia
Mandlhate alipokuwa akifungua semina ya inayohusu namna ya kuimarisha
mawasiliano na utoaji wa taarifa sahihi zinazohusiana na magonjwa ya
mafua makali katika ukanda wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika,
semina hiyo inayoendelea jijini Nairobi.
Mawasiliano ya haraka wakati wa
dharura za kiafya yanahusu ngazi zote kuanzia kimataifa wakati wa hatari
ni yetu sote, ni ya kimataifa, kikanda na kitaifa, hivyo basi
kipaumbele cha WHO ni kuhamasisha watu, mashirika na serikali kushiriki
katika kutoa taarifa na elimu juu ya namna ya kuokoa maisha ili kuchukua
hatua sahihi za kuzuia, kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho
ugonjwa huo” alisema Dkt. Custodia.
Dkt. Custodia alisema kuwa hatua
ya kupata elimu sahihi ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo
inatekelezwa kwa kupitia matumizi bora ya mawasiliano ya umma juu ya
afya, ushiriki wa jamii na uhamasishaji wa kijamii kwa kutumia vyombo
vya habari, sera na tafiti zinazofaywa ili kuokoa maisha ya watu katika
eneo husika.
Malengo ya mkutano huo ni
kuwajengea uwezo washiriki ambao utaimarisha mawasiliano kwa watoa
maamuzi muhimu ya kitaifa na kikanda katika kuimarisha hatua za dharura
katika kuzuia, kujikinga na kujilinda dhidi ya vitisho ugonjwa wa mafua
makali.
Malengo mengine ni pamoja na
washiriki kupata uelewa juu ya njia bora za kutoa taarifa wakati
inapotokea hatari ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababisha madhara
makubwa ya kiafya ambayo yanahitaji dharura katika utekelezaji wake
pamoja na kuimarisha mitandao ya kikanda ya watoa maamuzi na watendaji
ili kubadilishana uzoefu na utaalamu kupitia nchi wanazoziwakilisha.
Kwa upande wake muwakilishi
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania Dkt. Vida Makundi
alisema kuwa semina hiyo ina manufaa makubwa kwa taifa hilo kwa kuwa
nchi hiyo tayari ina viashiria vya kuapata yanayotokana na wanyama
yakiwemo mafua makali ya ndege na mengine hivyo hivyo ni vema kujifunza
na kuchukua tahadhari ikiwaa ni pamoja na kuelimisha jamii namna ya
kujikinga majanga mbalimbali ya magonjwa na matukio yanayoathiri afya ya
binadamu yanapotokea.
Dkt. Vida alisisitiza kuwa
wataalamu wa afya na sekta nyingine zinzohusika na afya ya binadamu
wakaelewa kuwa ili kufanikisha mawasiliano kwa jamii hawana budi
kushirikiana kwa karibu na wanahabari kutoa habari kwa jamii ili kuokoa
maisha ya watu kwa haraka unapotokea mlipuko wa magonjwa ambapo
kunahitajika kuwepo na uelewa mpana wa kisiasa, kijamii na kiutamaduni
na kuzingatia eneo lililoathiriwa na ugojwa wa mlipuko.
Mkutano huo unaoendelea Nairobi
nchini Kenya unaongozwa na kaulimbiu inayosema “Okoa maisha na zuia
ugonjwa kuenea” unajumisha ya zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi 21
zilizopo katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo
washiriki wanatoka katika Wizara za Afya, Habari na Muwakilishi mmoja wa
WHO kutoka nchi anayowakilisha katika ukanda huo.
Nchi hizo ni pamoja na Tanzania,
Uganda, Msumbiji, Malawi, Botswana, Lesotho, Sudani ya Kusini,
Madagaska, Visiwa vya Shelisheli, Comoro, Swaziland, Rwanda, Mauritius,
Eritrea, Namibia, Ethiopia, Afrika Kusini na Zimbabwe.na Kenya ambayo ni
mwenyeji wa semina hiyo.