MAGALULA AIPA SOMO BODI YA MAJENGO

September 18, 2015


 Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalula, akimulikiwa mwanga kwa kutumia tochi ya simu na mshiriki  wa kongamano hilo, Flavian Rugaimukamu kufuatia umeme kukatika mara kwa mara wakati akifungua kongamano la Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Ukadiriaji wa Majenzi uliofanyika mkoani Tanga



NA SALUM MOHAMED wa tangakumekuchablog
ALIEKUWA MKUU wa Mkoa wa Tanga ambaye amehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalulla, ameiagiza bodi ya Usajili wa Wabinu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, kuwachukulia hatua kali za kisheria wabadhrifu na wala rushwa ndani ya bodi hiyo.
Akifungua kongamano la 24 ya bodi ya Usajili Mkoani hapa leo, Magalula, alisema kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakivunja maadili ya kazi zao ikiwemo kujihusisha la ulaji rushwa jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma bodi hiyo.
Alisema ili kuweza kupiga hatua za kuwaletea maendeleo wananchi ni vyema bodi ya Usajili ikifanya ukaguzi mikataba ya makampuni kwa madai kuwa huko ndiko ubadhrifu unakoanzia.
“Jambo la faraja ni kuona wenyeviti wakuu wa taasisi na watendaji mbalimbali muko kwa pamoja hapa na hiki ambacho mutakijadili na kuadhimia kitakuwa cha faida kwa maslahi ya maendeleo ya wananchi” alisema Mgalula na kuongeza
“Ila jambo la msingi naiagiza bodi ya usajili wa ubunifu majengo kusafisha wala rushwa kila idara-----jambo hili limekuwa likirudisha nyuma jitihada za bodi” alisema
Alisema wala rushwa wamejificha kila idara na hivyo kuitaka bodi hiyo kufichua makucha yake kwa kuwafichua na kuwaweka hadharani ikiwa na pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Akizungumza katika kongamano hilo, Msajili wa bodi, Abdalla Jihad, alisema bodi hiyo imewachukulia hatua za kisheria wataalamu waliokiuka taaluma zao 92 na makampuni 57 yamefutiwa usajili kwa kukiuka sheria.
Alisema hatua hizo imesaidia kwa baadhi ya wataalamu kuzingatia maadili na nafasi zao ikiwa na pamoja na makampuni kuzingatia sheria za usajili jambo ambalo imekuwa msaada kwa bodi.
“Katika kusimamia sheria bodi imeweza kuwachukulia hatua za kisheria wataalamu tisini na mbili sambamba na makapuni 57 yaliyokiuka sheria” alisema Jihad
Alisema kwa mantiki hiyo bodi imejipanga kuhakikisha wataalamu wanazitumia nafasi zao na kuziba mianya yote ya rushwa na ubadhrifu wa pesa ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea.
                                                  Mwisho


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »