Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akizungumza na
wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini hawapo pichani wakati akifunga
mafunzo ya wiki nane ya ujasiriamali kwa wanafunzi hao mwishoni mwa wiki
jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliendeshwa chini ya mpango wa
Cambridge Development Initiative (CDI) ili kuimarisha mafunzo ya maswala
ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini. CDI ni mpango
ulioasisiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini
uingereza. Kulia ni Rais wa CDI, Ravi Solanki.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (katikati)
akikabidhi hundi ya dola 3000 kwa wanafunzi wawili kutoka chuo kikuu cha
Ardhi walioibuka washindi kwa wazo bora la biashara baada ya mafunzo ya
wiki nane ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na NEEC kwa ushirikiano na
mpango wa Cambridge Development Initiative (CDI) unaoendeshwa na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza. Wengine ni
Moses Mtei, mshindi (kushoto); Mkurugenzi wa Ujasiriamali CDI, Bi.
Georgia Ware (kulia); na Joel Kissava pia mshindi toka Chuo kikuu Ardhi
(wapili kulia). Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (wa pili
kushoto) akikabidhi hundi ya dola 3000 kwa mmoja wa wanafunzi walioibuka
washindi kwa wazo bora la biashara baada ya mafunzo ya wiki nane ya
ujasiriamali yaliyoendeshwa na NEEC kwa ushirikiano na mpango wa
Cambridge Development Initiative (CDI) unaoendeshwa na wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza. Wengine ni Bhoke Nyaisaba
toka UDSM, mshindi (kulia); Mkurugenzi wa Ujasiriamali CDI, Bi. Georgia
Ware (wa pili kulia); na mwanafunzi toka UDSM, Vivian Mushi (kushoto).
Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.