WAGOMBEA URAIS CCM NA HADITHI YA LIGI KUU BARA

June 13, 2015



Harakati za kutangaza nia kwa wagombe nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) limeshika kasi, hata hivyo wale wanaodhaniwa kuwa nguvu hakuna hata mmoja ambaye mkoa wake una timu katika Ligi Kuu Bara.


Ni kama wagombea hao wameikwepa ligi kuu ambayo ingeweza kutumika kama mtaji wa kisiasa kwao kwa kupata kura za wanamichezo.

Championi Jumamosi limewatazama baadhi ya wagombea hao CCM na hakuna hata mmoja ambaye jimbo au mkoa wake una timu ya ligi kuu au ambayo imepanda kucheza michuano hiyo msimu ujao.
Bernald Membe
Membe ni Mbunge wa Jimbo la Mtama lililopo mkoani Lindi pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Lindi haina timu katika ligi kuu na klabu yake ya mwisho kushiriki michuano hiyo ni Kariakoo Lindi ambayo ilishuka daraja miaka 12 iliyopita.

Stephen Wassira
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda mkoani Mara ametangaza nia ya kuwani nafasi ya urais. Polisi Mara ilishiriki ligi kuu mara ya mwisho miaka ya mwanzoni ya 2000, tangu hapo Mara haina katika ligi hiyo hadi leo.

Samuel Sitta
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Tabora, ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ametangaza nia ya kutaka kuwa rais wa Tanzania, hata hivyo mkoa wake hauna timu ligi kuu. Rhino Rangers ndiyo timu ya mwisho ya Tabora kucheza ligi hiyo msimu wa 2013/14.

Edward Lowassa

Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa ni miongini mwa watangaza nia wenye nguvu nchini lakini mkoa wake hauna timu ligi kuu. Mara ya mwisho watu wa Arusha kutazama mechi za ligi kuu pale kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ilikuwa msimu wa 2013/14 ambapo JKT Oljoro ilishuka daraja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »