Luiza
Mtafi wa NHIF akimpima mapigo ya moyo mmoja wa wananchama waliotembelea
banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonyesho ya tatu ya
biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako mjini
Tanga.
Afisa
Matekelezo wa NHIF Bi. Shazy Amasha akitoa elimu kuhusu bima ya Afya
kwa watoto waliotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika
maonyesho ya tatu ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja
vya Mwahako mjini Tanga.
Nesi
Anna Jengo wa hospitali ya Bombo akimpima kiwango cha sukari Bw. Ahmed
Ismail aliyetembelea katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
kupata huduma hiyo.
imu
ya Maafisa wa NHIF ikifurahia ushindi baada ya kushinda nafasi ya
kwanza katika kada ya afya kwenye maonyesho ya tatu ya biashara ya
kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako mjini Tanga.
…………………………………………………………………………………
Na Catherine Kameka
Mamia ya wananchi wa Mkoa wa
Tanga, wameendelea kujitokeza kwa wingi katika banda la Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF) ili kupima afya zao.
NHIF Mkoa wa Tanga kwa
kushirikiana na Makao makuu, inaendesha zoezi la upimaji afya bure kwa
wananchi wa Tanga na maeneo ya karibu ikiwa ni sehemu ya majukumu yake
ya kutoa huduma kwa wananchama wake na wananchi kwa ujumla.
“Lengo kubwa la NHIF ni
kuelimisha wananchama na jamii kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza
ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi”
Meneja wa NHIF Tanga Bw. Ali
Mwakababu aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya lililopo katika viwanja
vya Mwahako ambapo maonyesho ya tatu ya biashara ya kimataifa
yanafanyika.
Aliongeza kwa kusema kuwa katika
zoezi hili wanachama na wananchi wa mkoa wa Tanga watapimwa shinikizo la
damu (BP), sukari na uzito na urefu na kuainisha uwiano kati ya uzito
na urefu na watakaokutwa na matatizo watapata ushauri wakitaalamu na
madaktari wa Mfuko waliopo kwenye banda hilo.
Hivyo alitumia fursa hiyo
kuwaomba wakazi wa Tanga kuutumia muda huo kwa kujitokeza katika
viwanja vya Mwahako ili kupima afya zao.