Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini
Pemba linamshikilia mzee mwenye umri wa miaka 75 akikabiliwa na tuhuma
ya kupatikana na majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amemtaja mzee huyo kuwa ni
Hamad Hamad Bakar Mkaazi wa Mchangamdogo Wilaya ya Wete .
Amesema kuwa mzee huyo
amepatikana akiwa na nyongo 75 na mafurushi mawili ya majani makavu
yanayo sadikiwa kuwa ni bangi baada ya kufanyiwa upekuzi ndani ya nyumba
yake .
Ameeleza kwamba tukio hilo
limetokea juzi na kuongeza kuwa walipokea taarifa juu ya uwepo kwa
bangi katika nyumba ya mzee huyo kutoka kwa Polisi Jamii ambao
waliambatana nao kufanya upekuzi ndani ya nyumba hiyo .
Aidha Kamanda Shekhan amesema
kuwa jeshi hilo kwa sasa linaendelea kumhoji mzee huyo na atafikishwa
mahakamani upelelezi utakapo kamlika kwa ajili ya kujibu tuhuma
zinazomkabili .
“Ni kweli kwamba jeshi la Polisi
linamshikilia mzee Hamad Hamad Bakar baada ya kukamatwa akiwa na nyongo
75 pamoja na mafurushi mawili ya majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni
bangi na tutamfikisha mahakamani upelelezi utakapo kamilika ”
alifahamisha Kamanda .
Wakizungumza na mwandishi wa
habari hizi polisi Jamii katika Shehia hiyo wamesema kuwa bado vyombo
vya sheria ikiwemo Mahakama hazijakuwa tayari kushirikiana na polisi
kwani mzee huyo ameshakamatwa mara nyingi lakini kesi zake hazipatiwa
hukumu stahili
Wamesema kuwa mzee huyo
anaugonjwa wa Ukoma ni mzoefu wa biashara hiyo na kwamba amewahi
kukamatwa na kufikishwa mahakamani zaidi ya mara moja lakini hakuna
adhabu iliyochukuliwa dhidi yake .
“Hatuwezi kufanikisha udhibiti na
utumiaji wa dawa za kulevya iwapo watuhumiwa wanashindwa kuchukuliwa
hatua kwani huyu mzee si mara ya kwanza kukamatwa na bangi lakini hakuna
adhabu iliochukuliwa dhidi yake ” alifahamisha Kiongozi wa Polisi Jamii
.
Hivyo wameviomba vyombo vya
sheria kuhakikisha kwamba wanachukua hatua inayostahili ili kukomesha
biashara hii haramu ya madawa ya kulevya kwa lengo la kuwalinda vijana
dhidi ya majanga mbali mbali .
EmoticonEmoticon