KWA mara ya kwanza baada ya miaka
mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam,
kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati
Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
Wasanii wa yamoto band.
Ni onyesho ambalo limeteka hisia
za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili
havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale
matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.
Kesho, Ijumaa, Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’.
Vilevile, Twanga Pepeta ambao
hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa
Wenge Garden Ukonga. Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden
na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa
hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.
EmoticonEmoticon