Dkt. Mmbando akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana na mkataba huo toka serikali ya korea ya
kusini katika kutoa mafunzo kwa mafundi wa vifaa na vifaa tiba
walioajiriwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya hapa nchini ili
waweze kuongeza ujuzi katika matengenezo na kuboresha huduma ya
ufundi.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowele
Katibu
mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na naibu meneja toka KOFIH
wakisaini mkataba huo. Mkataba huo utasaidia pia kuboresha huduma za
ufundi wa vifaa tiba katika karakana za ufundi wa vifaa tiba zilizopo
katika hospitali za rufaa za kanda, rufaa za mikoa na hospitali za
wilaya.
Dkt. Mmbado akikabidhiwa mkataba huo toka kwa Naibu Meneja Gong, In Jae .
…………………………………………………………..
Dkt.
Mmbando amesema , serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya
imeendelea kuboresha upatikanaji na uwepo wa huduma ya vifaa tiba na
mashine mbalimbali za teknolojia za kisasa katika ngazi zote za vituo
vya kutolea huduma za Afya kuanzia zahanati hadi hospitali ya Taifa. Ili
kusimamia matumizi bora na kutunza raslimali hii kumehitajika kuweka
juhudi za maksudi kuandaa wataalam wa ufundi wa vifaa tiba kwa
kuwajengea uwezo katika kufahamu wa namna ya matengenezo ya mashine
zilizopo na zinazo endelea kununuliwa; Pia kuwapa vitendea kazi(tools
kits, measuring and calibration equipment) vyenye kuwezesha mafundi
kuhakiki ubora wa ufanyaji kazi kwa baadhi ya vifaa tiba mara baada ya
kufanyiwa matengenezo.
“Kwa
ushirikiano huu kati yetu na Korea ya Kusini ikiwa ni nchi iliyopiga
hatua kubwa kiuchumi na teknolojia au miundombinu kwa ujumla wake
ninaimani tutajifunza mambo mengi na kutoa mchango mkubwa katika
kuboresha huduma za afya hapa nchini”.
Alisema
kikubwa wamelenga kupata ujuzi zaidi kutoka kwao ingawa watagharimia
masuala mengi katika mchakato mzima. Tunahitaji sisi wenyewe serikali ya
Tanzania kupitia wizara ya Afya, Manispaa na Halmashauri zote nchini
kuhakikisha vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za Afya
vinapatikana na vinatumika kutoa huduma kwa wagonjwa muda wote
vinapohitajika.|” Hili litawezekana kama tutatenga bajeti za matengenezo
kinga(Planned Preventive maintenance) na kutumia wataalam wa ufundi wa
vifaa tiba wanaotambulika “.
EmoticonEmoticon