Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

March 12, 2015

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mheshimiwa Binilith Mahenge akisiliza jambo kutoka kwa Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abas Kandoro kabla ya kuanza Ziara yake ya siku mbili Mkoani humo jana. (Picha na OMR)
002
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge (katikati), wakijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mh. Deodatus Kinawito (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde (kulia) wakati wa Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani humo jana.
004
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge, akionesha Bwawa linalotumika kuhifadhi Maji-taka yenye Sumu kutoka kwenye Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya jana, huku akiwataka Wawekezaji wa Mgodi huo kuboresha Bwawa hilo ili kukidhi Kanuni za Mazingira za Tanzania . 
005
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Injinia Binilith Mahenge akisaini Kitabu cha Mahudhurio ya Wageni mbele ya Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abas Kandoro, kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo jana .
1111
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Machimbo ya Dhahabu katika Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya, Bwana Andy Wu (kulia), katika ziara ya Mazingira Mgodini humo jana na wakati katika picha ni Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »