Afisa
habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na
uzinduzi wa ripoti ya Kupambana na dawa za kulevya ya Umoja wa Mataifa.
Kulia ni mgeni rasmi Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya
Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC), January Ntisi na kushoto ni Afisa
Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma
Ledama.
Mchambuzi
Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (DCC),
January Ntisi akifafanua jambo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi
huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa kupambana utumiaji wa Madawa ya Kulevya waliohudhuria uzinduzi huo.
………………………………………………………………….
Na Andrew Chale wa Modewji blog.
Uongozi
wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataaifa (UNIC) umezindua ripoti ya
Kupambana na dawa za kulevyaa ya Umoja wa Mataaifa, Uzinduzi uliofanywa
Machi 4, Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza
mbele ya wandishi wa habari kwa upande wake, Afisa Habari wa Kituo Cha
Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alibainisha ripoti hiyo
imeweza kuchambua mambo mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya na mikakati
iliyofikiwa.
Ambapo
alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo ni pamoja
na kupungua kwa wimbi la kuingia kwa dawa za kulevyaa nchini hasa
kupitia njia za bahari ya Hindi huku mji wa Mexico wa America,
ukipunguza kwa asilimia kubwa matumizi ya dawa za kulevya.
Vuzo
alibainisha kuwa, pia mikakati iliyofikiwa ambayo pia imo kwenye ripoti
hiyo ni pamoja na mfumo wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya
wanaoacha kwa kuwapatia dawa maalum za kupunguza taratibu matumizi hayo.
‘Mipango
ya kuwapatia wale wanaocha dawa maalum za kusaidia utumiaji wa madawa
na pia dhidi ya kupambana na dawa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wa
watumiaji” alisema Vuzo.
Aidha,
alibainisha kuwa, Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza
kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya
Cocaine na Heroine .
Kwa
upande wake Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya kudhibiti
Ukimwi DCC, January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na
dawa za kulevya na umoja huo kwani Tanzania ni miongoni nchi ambazo pia
zinakabiriwa na tatizo hilo.
Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.
Kwa
upande wake, Immaculate Nyoni ambaye ni Project officer UNODC
alibainisha juhudi mbalimbali zinafanywa katika kukabiliana na wimbi la
dawa za kulevya duniani kote ambapo kwa sasa angalau matumizi hayo
yakiendelea kupungu
EmoticonEmoticon