Muonekano wa Daraja jipya la Salenda litaakalopita
baharini kuanzia Coco Beachi (Oysterbay) kwenda Hospitali ya Aga Khan
(Maeneo ya Ocean Road/ Baraka Obama Road). Daraja hilo pamoja na
barabara zake, litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na uwezo wa kupitisha
magari zaidi ya 61,000 kwa siku huku likiwa na njia nne za magari pamoja
service road njia za waenda kwa miguu kila upande
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
kulia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Chung Il wapili
kushoto kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Ujenzi pamoja
na mchakato wa Ujenzi wa Daraja jipya la Salenda litakalopita baharini. Wa
kwanza kushoto ni mke wa Balozi huyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe
kushoto akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea Chung Il kulia.
Katikati ni Eng. Consolata Ngimbwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi
nchini (CRB).
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
kushoto akimkabidhi zawadi Balozi wa Jamhuri ya Korea, Chung Il mara
baada ya hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Balozi huyo kwa
Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale
akikaribishwa na Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Korea. Kulia ni Balozi huyo
Chung Il.
Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS Eng. Victor Seff
akisalimiana na Mke wa Balozi.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea,
Masaki jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Korea ya Kusini hatimae imekubali kutoa fedha kwa
ajili ya kuanza Ujenzi wa Daraja jipya la kisasa la Salender. Daraja hili
litakuwa mbadala wa daraja la Zamani la Salender.
Serikali hiyo imekubali kutoa mkopo wa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa
Daraja hilo jipya na la kisasa kabisa litakalopita baharini pembezoni mwa
Daraja la zamani la Salender kuanzia Coco Beachi (Oysterbay) kwenda
Hospitali ya Aga Khan (Maeneo ya Ocean Road/ Baraka Obama Road).
Kauli hiyo ilitolewa na Balozi wa Jamhuri ya Korea ya Kusini nchini Ndugu
Chung Il wakati alipomwalika Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
pamoja na Ujumbe wake katika chakula cha jioni nyumbani kwake Masaki
jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, Balozi wa Jamhuri ya
Korea ndugu Chung Il alisema kuwa fedha hizo za mkopo wa masharti
nafuu zitatolewa kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yake na
Tanzania.
“Naomba tuendelee kudumisha uhusiano wetu hapa Tanzania pamoja na
Korea ya Kusini na ndio maana kuna wananchi zaidi ya 500 kutoka Korea
ya Kusini wanaoishi hapa Tanzania” alisema Balozi huyo wa Jamhuri ya
Korea ya Kusini.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea ya Kusini kwa kuridhia kutoa
fedha hizo kwa ajili ya kuanza Ujenzi wa Daraja hilo la kihistoria nchini.
“Naishukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Korea ya Kusini kwa msaada
mkubwa katika ujenzi wa Daraja hili jipya litakaloanzia maeneo ya Coco
Beachi (Oysterbay) kwenda Hospitali ya Aga Khan (Maeneo ya Ocean
Road/ Baraka Obama Road)..” Alisema Waziri Magufuli.
Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali hiyo ya Jamhuri ya Korea ndio
iliyowezesha pia ujenzi wa Daraja la Kikwete katika mto Malagarasi pamoja
na ujenzi wa barabara ya kilomita 48 mkoani Kigoma.
“Daraja la Kikwete mkoani Kigoma limekwisha kamilika pamoja na
barabara ya kilomita 48 kwa ubora mkubwa hivyo naamini kuwa hata
ujenzi wa daraja hili jipya la Salender litakalopita baharini litakuwa
mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki” Alisema Waziri
Magufuli.
Daraja hilo jipya pamoja na barabara, litakuwa na urefu wa kilomita 7.2
na uwezo wa kupitisha magari zaidi ya 61,000 kwa siku. Ujenzi wa Daraja
hilo utaanza mwaka huu na wiki ijayo makubaliano kwenye makabrasha
ya kimkataba yatamalizika. Daraja hilo litakuwa na njia nne za magari
pamoja service road njia za waenda kwa miguu kila upande. Mara baada
ya kukamilika kwake daraja la zamani la Selander litaendelea kutumika
kama kawaida sambamba na Daraja jipya la Salender.
Hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Balozi wa Jamhuri ya
Korea ndugu Chung Il ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi Eng. Musa Iyombe, Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi nchini
Eng. Consolata Ngimbwa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini
TANROADS, Eng. Patrick Mfugale pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Miradi
wa TANROADS Eng. Victor Seif.
EmoticonEmoticon