Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………………………
Wajasiriamali na
wakulima hapa nchini wametakiwa kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye
ubora zitakazofaa kwenye masoko ya uhakiki sanjari na kuweza kuyamudu
masoko kwani hilo limekuwa ndio tatizo la wajasiriamali wengi kutoweza
kuandaa bidhaa kwa ubora.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa
Chuo cha Veta Mkoani hapa Banga Deusdedit wakati akifunga maonyesho ya
wauzaji wa bidhaa za kilimo na mikopo yaliofanyika kwa siku tatu jijini
hapa na kumalizoika mwishoni mwa wiki.
Banga alisema kuwa malengo ya
maonyesho hayo ya EFTA na dhamira yao iwe chacu kwa wajasiriamali ambao
wamepata mafunzo mbalimbali ya kuweza kujiajiri na kuweza kuzalisha
bidhaa zenye ubora na uhakika kwenye masoko ya ndani na nje.
Aliongeza kuwa unapukuwa na soko
la uhakika na bidhaa zenye viwango vyenye ubora huhitaji kutumia nguvu
kuitangaza kwani kuna msemo wa Kiswahili kibaya kinajitembeza kizuri
kinajiuza hivyo mzalishe bidhaa zenye ubora zitakazopata soko la
uhakika.
“Mara nyingi nimekuwa nikangalia
maonyesho mbalimbali ya wajasiriamali na wamekuwa wakionyesha bidhaa
mbalimbali wanazozalisha lakini hazipo kwenye masoko ya uhakika ni
wajibu wenu mkatumie mafunzo haya mliopata kuhakikisha mnayasogelea
masoko ya uhakika”aliongeza Banga.
Mmoja wa washiriki wa maonyesho
hayo kutoka Tanzania Farmers Service Center Faustine Urio aliwataka
watanzania kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora wa uhakika na
kuhakikisha wanauwezo wa kuhudumia masoko yao kwa uhakika bila ya
kukatisha bidhaa kwenye masoko.
Urio alisema kuwa kampuni yao
imejipanga kuhakikisha wanawalitea watanzania bidhaa na vifaa vyenye
viwango vya kisasa vitavyowasaidia kuzalisha na kutengenea bidhaa zenye
ubora na kuhakikisha Maendeleo kwa watu wa kada hiyo yanapatika kwa
uhakika.
“TFSC kama mlivyoona tulikuwa
tunaonyesha na kukopesha aina m,bali mbali za matrekta na vifaa vya
kilimo vitakavyowasaidia wakulima na wajasiriamali kuweza kufikia
malengo waliojiwekea na washauri mtumie bidhaa zetu”alisema Urio.
EmoticonEmoticon