Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia),
akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan
Mmbando, moja ya kompyuta na baadhi ya vifaa tiba vyenye thamani ya dola
za Marekani 46,000 vilivyotolewa na WHO kwa Serikali ya Tanzania Dar es
Salaam leo, kwa ajili ya maandalizi ya udhibiti wa magonjwa ya
kuambukiza na ebola.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia),
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando
wakitiliana saini za makabidhiano ya vifaa hivyo.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia),
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando
wakibadilishana hati baada ya kusaini makabidhiano ya vifaa hivyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando akionesha
pampu ya kupulizia dawa kwa mbali za kutibu magonjwa ya kuambukiza.
Wadau wa sekta ya Afya wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa vikiwa katika maboksi.
Na Dotto Mwaibale
……………………………………………..
SHIRIKA
la Afya Duniani (WHO), limetoa msaada wa vifaa tiba kwa Serikali ya
Tanzania vyenye thamani ya dola la marekani 46,000 kwa ajili ya
maandalizi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na ebola.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kupokea msaada huo jijini Dar es Salaam leo Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Donan Mmbando alisema
vifaa hivyo vimefika wakati muafaka wakati serikali ikiwa katika mpango
maalumu wa kuiandaa nchi kukabiliana na magonjwa hayo.
“Tunalishukuru
shirika la WHO kwa msaada huu mkubwa waliotupatia kwani utatusaidia
katika kukabiliana na magonjwa hayo hasa wa ebola ambao umeenea zaidi
Afrika Magharibi” alisema Dk.Mmbando.
Alisema
ilikukabiliana na changamoto ya magonjwa hayo Serikali imetoa mafunzo,
kuimarisha maabara za utambuzi wa viashiria vya ugonjwa huo pamoja na
vifaa tiba mbalimbali.
Alisema
utambuzi wa viashiria vya ugonjwa huo vinafanyika katika maabara kubwa
iliyopo katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya pamoja na Muhimbili.
Dk.
Mmbando alisema tangu ugonjwa huo uibuke katika nchi kadhaa za Afrika
Magharibi umewaathiri watu 23,000 pamoja na kusababisha vifo vya watu
9,000.
Akikabidhi
msaada huo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO), Rutaro
Chatora alisema shirika hilo limekuwa likisaidia misaada ya huduma za
afya katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi za Guinea, Liberia na Siera
Leon.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
EmoticonEmoticon