NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM.
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) kesho
jumamosi itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo
utakaoanza majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani
jijini Dar es salaam.
Wageni timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kutoka nchini Kenya wanatarajia
kuwasili leo jioni jijini Dar es salaam, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo huo
wa marudiano siku ya jumamosi na watafikia katika hoteli ya Saphire iliyopo
eneo la Gerezani – Kariakoo.
Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mombasa, timu
ya Taifa ya Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3 dhidi ya wenyeji
timu ya Taifa ya Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele
katika hatua inayofuata.
Waamuzi wa mchezo huo watakua ni , Beye Mbokh kutoka Senegal, mwamuzi wa
pili ni Signate Youssouph (Senegal), mwamuzi wa tatu, Maolidy Tsaralaza kutoka
Madagascar, mtunza muda (time keeper) atakua Hachim Said Nassur (Madagascar) na
kamishina wa mchezo atakua Roch Henriette kutoka Visiwa vya Shelisheli.
Tayari waamuzi wa mchezo huo wameshawasili jijini Dar e salaam tangu jana
jioni tayari kwa mchezo huo, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itasonga
mbele, itakutana na timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na kurudiana kati
ya Machi 13, 14, 2015.
Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa
kufanayika mapema mwaka huu katika Visiwa vya Shelisheli.
EmoticonEmoticon