Balozi
wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaki Okada akizumgumza na Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma
Kikwete pamoja na uongozi wa Taasisi hiyo muda mfupi kabla ya kutiliana
saini mkataba wa mradi wa kupanua Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama
iliyoko Rufiji, Mkoani Pwani tarehe 19.2.2015.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akitiliana saini na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa
Masaki Okada kwenye mradi wa upanuzi wa Shule ya Sekondari
WAMA-Nakayama utakaogharimu dola za kimarekani 498,738. Sherehe ya
utiaji saini ilifanyika kwenye ofisi za WAMA zilizopo karibu na Ikulu
ntarehe 19.2.2015.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana hati za
Mkataba na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara
baada ya kutia saini zao kwenye mkataba huo.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akizungumza mara baada ya
kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa upanuzi wa Shule ya WAMA
Nakayama.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada
ya viongozi hao kutia saini mkataba wa upanuzi wa Shule ya Sekondari
WAMA-Nakayama.
PICHA NA JOHN LUKUWI
EmoticonEmoticon