Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib
Bilal kuhusu Mzani wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao
umekamilika kwa asilimia 99.8.
Mzani
wa Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa
haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya
sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed
Gharib Bilal akihutubia wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya
kuukagua.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed
Gharib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa barabara ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha
lami.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya
kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani
walioathirika na kimbunga kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba
zaidi ya 40 katika kijiji hicho pekee.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akicheza ngoma pamoja na kikundi cha
ngoma cha Msoga kusherehekea ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa yenye
urefu wa km 10. Barabara hiyo itapunguza msongamano wa magari katika
eneo la Chalinze.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed
Gharib Bilal akisalimiana na watumishi wa TANROADS mara baada ya kukagua
Mzani wa Vigwaza.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu
ambaye pia ni Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi
wa Mzani wa Vigwaza.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli wakielekea kwenda kumpokea Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt.
Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mzani wa Vigwaza mkoani Pwani. Picha
zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya
Ujenzi
EmoticonEmoticon