Atletico Madrid itamtoa beki wake kisiki JoĂŁo Miranda
kwa moja ya vilabu vya Ligi Kuu ya England katika dirisha dogo la
usajili la Januari, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Star.
Manchester
United inatajwa kuwa mlengwa mkuu wa usajili huo ambapo Luis van Gaal
anatarajiwa kuongoza mbio za vilabu vya Ligi Kuu katika kuwania saini ya
beki huyo wa Kibrazil.
Miranda
mwenye umri wa miaka 30, amekuwa nguzo ya Atletico Madrid tangu
ilipomsajili Januari 2011, lakini sasa inaonekana wazi kuwa klabu hiyo
haina ubavu wa kuendelea kuwa na mchezaji huyo.
EmoticonEmoticon