Waziri wa
Uchukuzi nchini Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe amewafukuza kazi
wafanyakazi 6 wa Shirika la Reli nchini (TRL) kwa makosa ya wizi wa
fedha na ameamuru wakamatwe kuanzia leo na wafunguliwe mashtaka mara
moja.
Akiongea
Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo yake na wafanyakazi wa TRL
waliopeleka malalamiko ofisini kwake kuhusiana na uonevu wanaofanyiwa,
Dkt. Mwakyembe amesema waliofukuzwa kazi ni pamoja na kiongozi
anayehusika na kukata tiketi pamoja na wafanyakazi wa kawaida watano kwa
makosa ya kukatisha tiketi feki.
Dkt.
Mwakyembe amesema uchunguzi bado unaendelea kubaini wafanyakzi wengine
wanaokiuka sheria na taratibu za kazi zinazopelekea kudhoofisha ufanisi
wa shirika hilo linalotoa huduma ya usafiri wa reli ya Kati nchini.
Lakini
kufuatia uamuzi huo wa waziri wa uchukuzi, Katibu mkuu wa chama cha
wafanyakazi wa Reli Tanzania TRAU Erasto John Kiwele amesema kwamba
hawajaridhishwa na maamuzi yaliyochukuliwa na waziri kwa sababu
watuhumiwa wakuu wameachwa na kukandamizwa wadogo.
Wakati
huo huo, Wizara ya Uchukuzi imetolea ufafanuzi tukio la kuvunja kwa
jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam, kulikosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha juzi
katika jiji hilo.
Akitolea
ufafanuzi suala hilo katika mahojiano maalum na Hotmix, waziri wa
Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe amekiri kutokea kwa hali hiyo na kusema
kuwa serikali ina mpango wa kulibomoa jengo, na tayari ujenzi wa jengo
jipya litakalokuwa likitumika kwa kazi hiyo umekamilika.
Akizungumzia
tatizo la usafiri wa majini kati ya miji ya Mwanza na Bukoba baada ya
kuisimamisha meli ya MV Victoria, Dkt Mwakyembe amesema Meli ya MV
Serengeti yenye uwezo wa kubeba abiria 500 na mizigo tani 385 itachukua
nafasi ya MV Victoria iliyokuwa ikibeba abiria 1200, ambayo
imesimamishwa kwa ajili ya matengenezo.
EmoticonEmoticon