Majira ya saa moja asubuhi katika kituo cha Mandara ikiwa ni siku ya pili ya safari ya Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro maandalizi ya muendelezo wa safari hiyo yanaanza. |
Balozi wa Tanzania katika falme za nchi za kiarabu,Mbarouk N. Mbarouk akiongoza msafara wa Mabalozi kuelekea kituo cha Horombo. |
Sfarai inaendelea. |
Balozi Adadi Rajab anayeiakilisha Tanzania nchini Zimbabwe na Mauritius akitafakari safari ya kuelekea kituo cha Horombo. |
Mabalozi Patrick Tsere (Malawi) na Balozi Batilda Burian wakivuta pumzi kwanza kabla ya kuendelea na safari. |
Balozi Grace Mujuma (Zambia) akiongozana na Balozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Balozi Charles Sanga wakienda na mwendo wa Mdogo mdogo. |
Muongoza watalii mkuu msaidizi wa kampuni ya Zara Tour ,Theofiri(mwenye miwani) akiwaongoza mabalozi kuelekea kituo cha Horombo. |
Mabalozi ,Waandishi pamoja na waongoza watalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea kwa umbali mrefu kueleka Horombo. |
Safari ya kuelekea kituo cha Horombo ikaendelea kwa pamoja bila ya kuacahana. |
Mahala pengine Mabalozi walilazimika kutumia fimbo maalumu kupanda maeneo ambayo yalkuwa na vipando vikali. |
Mabalozi ,Shamim Nyanduga( Msumbiji) na Radhia Msuya (Afrika Kusini) walilazimika kupaka mafuta mgando katika nyuso zao ili kuzuia kubabuka na jua. |
Balozo Tsere akipatiwa huduma ya kwanza ya kuchuwa mguu wake ili aweze kuendelea na safari ,kulia ni balozi Batilida Buriani. |
Balozi Mwinyi aliamua kupoza koo huku akitafakari safari hiyo. |
Kila mmoja aliamua kupumzika ili kuvuta nguvu ya kumalizia kipande kilichokuwa kimebakia. |
Maeneo mengine mabalozi walifanya mazungumzo na wageni waliokuwa wakishuka toka kileleni. |
Hatimaye Mabalozi wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata chakula . |
Wale waliokuwa wamepungukiwa maji waliongezewa kwa kuwa ndio dawa pekee ili kufanikisha kuwez kupanda Mlima Kilimanjaro. |
Safari ikaendelea. |
Hataimaye kituo cha Horombo kikaonekana kwa mbali na mabalozi walitembea na kupumzika hapo. |
EmoticonEmoticon