KAMA ULIKOSA KUSOMA STORI HII KUHUSU TAHARUKI ILIYOJITOKEZA JENGO ALA BANDARI TANGA IPATE HAPA.

December 07, 2014

HUDUMA  za Kijamii Katika  Ofisi mbalimbali zilizopo kwenye Jengo la Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga zimesimama kwa masaa matatu  baada ya kutokea hali ya taharuki ya kishindo na kupasuka sakafu katika chumba kimoja kilichopo kwenye Jengo hilo.

Ofisi iliyotokea na kishindo hicho na kupelekea kupasuka iliyopo
ghorofa ya tatu iliyokuwa imepangishwa na kampuni ya mizingo ya Cargo Stars.

Akizungumza na TANGA RAHA BLOG ,Meneja wa Kampuni ya Cargo Stars  Tawi la Tanga,Godlisen  Mushi alisema kuwa wao walishtushwa sana na hali hiyo kutokana na kuwa kitendo hicho hakijawahi kuwakuta tokea wapipopoangisha ofisi hiyo.

  “Nilikuwa nimekaa ofisini nikiendelea na kazi zangu lakini ghafla nikasikia tetemeko kwa chini hali ambayo ilinilazimu kuacha kufanya kazi kwa muda mpaka wafanyakazi wenzangu na wengine tulipokutana na baadae tukarudi kwenye ofisi zetu “alisema Mushi.

Kwa upande wake,Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mkoa wa Tanga,Bertha Mwambela alisema kuwa wao walipokea tukio hilo kwa mshukto mkubwa hali ambayo iliwalazimu kutoka nje ya ofisi yao mpaka hapo hali hiyo ilipotulia na kurejea ofisini kwake.

Mwambela aliishauri mamlaka ya Bandari Mkoa wa Tanga,kuangalia uwezekano wa kuangalia namya ya kuvifanyia ukaguzi mara kwa mara nyumba viliyopo kwenye jengo hilo.

Akizungumzia tukio hilo,Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Tanga,Fredy Liundi alisema kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi ambapon tails zilizopo kwenye chumba hicho kilipasuka na kunyanyuka juu kutokana na uzito wa vitu vilivyokuwepo kwenye chumba hicho.

   “Kutokana na taharuki hiyo asilimi 60 ya wafanyakazi kwenye ofisi zilizopo kwenye jengo letu walitoka nje kwa ajili ya kujihami “Alisema Kaimu Meneja Fredy Liundi

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »