28/11/2014.
Serikali
imesema kuwa VICOBA ni taasisi binafsi inayomilikiwa na wananchi
wenyewe vikiwa ni miongoni mwa tasisi ndogo za kifedha ambazo ni za
kibinafsi na huanzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa ama kijijini,
kitongojini na hata kwenye kata.
Hayo
yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu
Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rungwe Magharibi Prof.
David Mwakyusa (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali inatambua VICOBA kama mkombozi wa wanyonge.
Mwigulu amefafanua kuwa taasisi hizo zimo kwenye sekta ya fedha isiyorasmi na zinatoa huduma za kifedha mijini na vijijini.
“Uwepo
wa taasisi hizi, umewezesha kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi
waliombali na huduma za sekta rasmi ya fedha na hivyo kuwa mkombozi wa
wanyonge” alisema mwigulu.
Aidha,
kwa kutambua suala hilo, ili kusaidia na kuimarisha taasisi hizo,
Mwigulu amesema kuwa Serikali baada ya kupata ushauri kutoka kwa Mshauri
Mwelekezi wa masuala ya uchumi na tafiti za kijamii, inafanya mapitio
ya Sera ya Taifa ya Taasisi ndogo za huduma ya fedha ya mwaka 2000 ili
kuihuisha iweze kukabili na kuzingatia mabadiliko na maendeleo
yanayojitokeza katika sekta hiyo.
Vilevile
Mwigulu amesema kuwa Serikali inakamilisha uhuishaji wa sera ya taasisi
ndogo ndogo za kifedha ambapo hatua inayofuata ni kuandaa mapendekezo
ya muswada ambayo yatapelekwa Baraza la Mawaziri mara baada ya kupata
idhini na maelekezo ya Baraza hilo na muswada huo utafikishwa bungeni.
Taasisi
ya VICOBA ilianzishwa nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo imekuwa
na manufaa kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini hususan wanawake
waishio vijijini wamefanikiwa kuboresha kipato chao na maisha yao kwa
ujumla kwa kujiunga na taasisi hiyo.
EmoticonEmoticon