Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania
imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda
Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya
Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili.
Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria
wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema
baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh
Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali
ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine
ya madai ya uchochezi, Mkoani Morogoro inayomkabili.
(PICHA/HABARI : DEOGRATIUS MONGELA/GPL)
Wakili wa Sheikh Ponda, Bw Juma Nassoro akizungumza jambo na mteja wake mahakamani hapo.
…. Nassoro akiteta jambo na Sheikh Ponda.
Askari akidumisha ulinzi mahakamani hapo.
Sheikh Ponda akitoka nje ya
Mahakama Kuu baada ya kushinda Kesi ya Ardhi iliyokuwa ikimkabili kisha
kurudi mahabusu katika gereza la Segerea.
….akipanda Karandinga la magereza.
Sheikh Ponda akiwa ndani ya gari la magereza tayari kwa kurudi rumande.
EmoticonEmoticon