Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na
Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu na Balozi wa
China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing wakikata Keki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu
kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na
Uwezeshaji Dkk. Mary Nagu akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya
kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar
es Salaam.
Picha ya Keki kwa ajili ya hafla ya maadhimisho ya
miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hafla hiyo imefanyika
jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing
(katikati) akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya
kuadhimisha miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Afisa anayeshughulikia masuala ya Menejimenti
na Programu wa Aga Khana Development Network Bw. Navroz Lakhani
Msanii wa Jamhuri ya Watu wa China akicheza mchezo
wa Wushu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri
ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
ya wageni wakisoma vitabu wakati wa hafla ya
kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni wakifuatilia michezo mbalimbali
kutoka kwa wasanii wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa
Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM
*************************************************
Na: Daud Manongi, WHVUM
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 China imetoa
msaada wa zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1.943 kwa ajili ya kusaidia
miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ushirikiano wa kibiashara dola bilioni 3.7 na uwekezaji dola bilioni
2.5 na jumla ya makampuni 500 yamewekeza nchini Tanzania.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Nci ofisi ya Waziri
Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu aliyekuwa mgeni rasmi katika
hafla ya miaka 65 ya toka kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini
Dar es Salaam.
Dkt Nagu amesema kuwa msaada huo utasaidia katika
kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwema Bandari ya Bagamoyo, mradi wa EPZ,
usambazaji wa umeme ukanda wa Kaskazini – Mashariki, Elimu kwa njia ya
mtandao,Serikali Mtandao kwa ajili ya Zanzibar na Umeme wa upepo katika mkoa wa
Singida.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua
njia za uchumi na kusababisha Tanzania kuwa na uchumi imara na endelevu.
“Najisikia faraja kusema kuwama pamoja na mafanikia
chanya tunayopata Tanzania bado ina miradi mingi ambayo inahitaji msaada wa
kifedha na kitaalam kutoka kwa Jamhuri ya Watu wa China na ni imani kuwa
wataendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha miradi hiyo” Alisema Dkt.
Nagu.
Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini Balozi
Lui Youqing amesema kuwa nchi yake itaendelea kuisaidi Tanzania kwa kuwa
kumekuwa na mahusiano mazuri nay a muda mrefu baina ya nchi hizi mbili.
Balozi Youqing ameongeza kuwa Tanzania inavutia
wakezaji kwa kuwa na mazingira salama ya kisiasa na kijamii ambapo
anashawishika kuunganisha wawekezaji wa China kushirikiana na wawekezaji
wengine katika kupunguza umasikini na kuleta maendeleo akitolea mfano
ushirikiano katika sekta ya majengo.
“Tanzania ni nchi kubwa yenye maono na inayovutia
zaidi kimataifa kutokana na uimara wake katika Nyanja za siasa na uchumi jamii,
imekuwa na ushawishi wa hali ya juu katika anga za kikanda na kimataifa, hali
inafanya wawekezaji kutoka sehemu kama EU, US, Japana na kwingineko waongeze
uwekezaji, ata mimi binafsi nashawishika kuwashawishi wawekezaji wa China
kuwekeza zaidi katika nchi hii” Alisema Balozi Youqing.
EmoticonEmoticon