Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi,Profesa Anna Tibaijuka kuingilia kati mgogoro wa uvamizi eneo lao ili kuepusha
uwezekano wa kutokea uvunjifu wa amani.
Walisema eneo lao ambalo walimilikishwa na Halmashauri ya Jiji la
Tanga tangu 2008 ,limevamiwa na Serikali ya Kijiji cha Kichangani na kugawa kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kinyume cha sheria.
Katibu wa kamati ya walimiki hao wa viwanda ya kushughulikia mgogoro huo,Kassim Salim alisema jana kuwa umefikia hatua mbaya na sasa kuna hatari ya kumwagika damu kwa sababu vijana wa Kichangani wanazuia wamiliki wa viwanda kujenga hapo.
“Baadhi tunataka kujenga viwanda lakini kuna vijana wamekuwa wakizuia magari kumwaga mawe na mchanga,ina maana wamejipanga kwa vurugu sasa hii hali inatakiwa kuingiliwa kati”alisema Salim.
Katibu huyo alisema tayari wamiliki hao wamefikisha malalamiko yao
katika ngazi mbalimbali za Halmashauri ya Jiji na Serikali Wilaya ya
Tanga lakini kuna hali ya kutegeana kutoa maamuzi jambo ambalo
linaweza kuhatarisha hali ya amani katika eneo hilo.
Alisema ili kuleta hali ya amani katika en eo hilo wameona ni vyema kumuomba Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Anna Tibaijuka kuingilia kati.
Mwenyeikiti wa Serikali ya Kijiji cha Kichangani,Rajab Mbalazi alisema kimsingi katika eneo hilo hakuna mgogoro kwa sababu ni mali ya Kijiji na imeamua kugawa kwa wananchi kwa kufuata taratibu zake na kwamba,wamiliki hao waligawiwa kinyume cha sheria kwani si mali ya Halmashauri ya Jiji.
“Mwaka 2008 Halmshauri ya Jiji la Tanga kupitia idara yake ya mipango ilichukua ardhi hiyo kinyemela bila ridhaa ya kijiji ndipo mwaka 2012 kupitia mkutano mkuu wa kijiji ukaamua kurejesha ardhi yake”alisema Mbalazi.
Mwenyekiti huyo alisema kuanzia Julai 28 mwaka 2012 Serikali ya kijiji iliamua kutekeleza kwa vitendo na karibu asilimia 90 ya ardhi
iliyokuwa imechukuliwa na halmashauri ya jiji kinyemela tayari
imeshagawa kwa wananchi.
Hata hivyo gazeti hili linayo nakala ya tangazo lililotolewa na
Halmashauri ya Jiji la Tanga lililosainiwa na Mkurugenzi
Mtendaji,Juliana Malange likitahadharisha kwamba kumejitokeza watu au kikundi chenye tabia ya uvamizi katika viwanja katika maeneo ya Kange A,B,C,D,E,F na Kange eneo la Viwanda ,Masiwani shamba,Mwakidila,Mwahako, Magaoni,Mwambani,Mbugani na EPZ.
Tangazo hilo liliwatahadharisha wananchi kuepuka kununua ovyo viwanja ambavyo havina nyaraka halali huku likiwahimiza wenye viwanja kuvilinda.
EmoticonEmoticon