Mahakama ya Rwanda inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa
ilioko mjini Arusha Tanzania, imethibitisha hukumu ya kifungo cha
maisha kwa viongozi wa zamani wawili kwa uhalifu wa mauaji ya
kimbari yaliofanywa mwaka wa 1994.
Matthieu Ngirum-patse na
Edouard Karemera, mwanachama wa zamani na naibu kiongozi wa
chama kilichotawala wakati huo, walihukumiwa kifungo cha maisha
mwaka wa 2011.
Walishitakiwa kuhusiana na mauaji ya halaiki,
uhalifu dhidi ya binaadamu na kwa kutozuwiya mauaji au kulaani
uhalifu huo uliotekelezwa na wanamgambo wa chama hicho
wanaojulikana kama Interahamwe.
Viongozi hao wawili walikuwa
wamekata rufaa katika kesi hiyo. Watu wanaokadiriwa kufikia
800,000 wengi wao kutoka kabila la wachache la watutsi waliuwawa
katika mapigano hayo yaliodumu siku 100 mauaji yaliosemakana
kuwa ya kasi mno kuliko yale ya wayahudi yaliotokea katika vita vya
pili vya dunia.
Viongozi hao wawili wa zamani nchini Rwanda
watabakia kizuizini wakisubiri kuhamishwa katika magereza ya nchi
nyengine watakapotumikia vifungo vyao. Serikali ya Rwanda
imepongeza uamuzi huo.
EmoticonEmoticon