Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya
Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa
Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria
mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya
maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa
vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.
Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New
York tarehe 22.9.2014.
Baadhi
ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa
Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama
Salma Kikwete.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller
(kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa
ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia
masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi
sahihi ya kiafya.
EmoticonEmoticon